Afisa ambaye anashughulikia masuala ya dhuluma za kijinsia kwenye kituo cha Polis cha Hindi kaunti ya Lamu Esther Jeffa ametoa wito kwa wazazi eneo hilo kufuatilia mienendo ya watoto wao hasa wakati huu wako kwenye likizo ndefu ya mwezi Disemba.
Amesema wazazi wanapaswa kuwa karibu na watoto wao ili kuwadhibiti dhidi ya visa vya dhuluma za kijinsia ambavyo vinaendelea kushuhudiwa eneo hilo.
Kulingana na Esther kumekuwa na visa vingi vya dhuluma mbalimbali katika eneo hilo la Hindi dhidi ya watoto wadogo, kesi ambazo zimekuwa zikiripotiwa kila mara katika kituo hicho cha polisi.
HIMIZO LATOLEWA KWA WAZAZI ENEO LA HINDI KUFUATILIA MIENENDO YA WATOTO WAO

