Idadi kubwa ya akina mama kaunti ya Kilifi inadaiwa kutohudhuria vikao vya kutoa maoni kuhusiana na miradi ya serikali ya kaunti, kutokana na kile ambacho kinadiwa nakala zinazotumika katika vikao hivyo huchapishwa kwa lugha ya kingereza.
Haya ni kwa mujibu wa mwanaharakati wa kutetea haki za watoto pamoja na wanawake kaunti ya Kilifi, Helda Lamek pamoja na Rose Chandugu, ambao wamesema ipo haja ya nakala hizo kuchapishwa kwa lugha ya Kiswahili ili wenyeji waweze kusoma na hata kuelewa kilichomo.
Wakizungumza katika kikao kilichoandawaliwa na shirika la Kilifi Citizen Forum na pia kilichowahusisha maafisa wa serikali ya kaunti ya Kilifi, wamesema iwapo zitachapishwa kwa lugha ya kiswalihi, kila mwananchi atafahamu kile kinachoendelezwa na serikali ya kaunti ya Kilifi.
Kwa upande wake kiongozi wa watu wenye uwezo maalum eneo la Malindi, Emmanuel Oguttu amelalamikia suala la walemavu kutengwa katika vikao hivyo na kusema kuwa ipo haja ya sheria za vikao hivyo kuzingatia asilimia Fulani ya walemavu, watakohudhuria vikao hivyo jambo ambalo limeungwa mkono na kiongozi wa vijana Joel Dzanga.
IDADI KUBWA YA KINA MAMA YADAIWA KUTOHUDHURIA VIKAO VYA KUTOA MAONI

