Gavana wa kaunti ya Tana River Dhadho Godhana amesema kongamano la nne la uchumi wa raslimali za baharini limekuwa lenye manufaa mengi.
Kulingana na Dhadho kongamano hilo la siku tatu ambalo lilikamilika siku ya Jumamosi eneo la Hola kaunti ya Tana River limewavutia washiriki wa kitaifa na kimataifa.
Amesema kongamano hilo limetoa fursa nzuri za uwekezaji kwa Tana River na kanda ya pwani kwa jumla.
Naye afisa mkuu mtendaji wa muungano wa jumiya ya kaunti za Pwani Emmanuel Nzai amesema wameorodhesha miradi ambayo wanapania kuitekeleza kwenye kaunti za pwani.
GAVANA DHADHO GODHANA APONGEZA KONGAMANO LA NNE LA UCHUMI WA RASLIMALI ZA BAHARINI

