Seneta wa kaunti ya Tana River Danson Mungatana ameitaka jumuiya ya kaunti za pwani kuwekeza pakubwa katika kaunti ya Tana River kama vile inavyowekeza katika kaunti zengine ukanda wa pwani.
Akizumgumza mjini Hola kaunti ya Tana River kwenye kongamano la nne la uchumi wa raslimali za baharini (BLUE ECONOMY) Mungatana amesema kunapaswa kuwa na miradi mbalimbali ambayo inapaswa kutekelezwa katika kaunti ya Tana River ila inafanywa jijini Nairobi licha ya kuwa miradi hiyo inawalenga wapwani.
Amesema miradi kama ya kuimarisha sekta ya uvuvi inapaswa kuwekezwa zaidi kanda ya pwani.
Wakati huohuo gavana wa Tana River Dhadho Godhana ameunga mkono kauli ya Mungatana na kuinyoshea kidole cha lawama serikali ya kuu kwa madai imechangia kwa sekta ya uvuvi kudorora kwenye kaunti hiyo na kanda ya pwani kwa jumla.
SENETA DANSON MUNGATANA AITAKA JUMUIYA YA KAUNTI ZA PWANI KUWEKEZA TANA RIVER

