ANGELLA OKUTOYI KUSHINDANISHWA NA MABINGWA WA RIADHA

Kinda wa kimataifa katika mchezo wa tenisi mwite Angella Okutoyi ameorodheswa kati ya wanariadha watakao ngangania taji la mchezaji bora wa mwaka wa kenya, tuzo zitakazofanyika mwezi januari mwaka 2023.

Hafla hiyo itafanyika katika kaunti ya Nairobi na makala ya mwaka huu yanahusisha pia kitengo cha wachezaji ambao bado ni wanafunzi baada ya kitengo hicho kuondolewa katika makala yalopita kutokana na kusitishwa kwa michezo ya shule katika katika kipindi cha janga la korona.

Okutoyi ambaye ni mkenya wa kwanza kushinda taji la Wembledon anashindanishwa na bingwa wa riadha za dunia Faith Kipgegon, bingwa wa mashindano ya jumuiya ya madola Mary Moraa na Betreace Chebet pamoja na nguli wengine akiwemo mshindi wa Boston Marathon Peres Jepchirchir