GAVANA WA MOMBASA AMEAHIDI KUSHIRIKIANA NA IDARA YA USALAMA

Gavana wa kaunti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir ameziomba asasi za usalama pamoja na Viongozi kaunti ya Mombasa kufanya kazi pamoja ili kuimarisha Usalama.
Akizungumza kwenye kikao kilichowaleta pamoja viongozi wa kisiasa kaunti ya Mombasa na maafisa wa Usalama katika eneo bunge la Nyali Nassir amesema hali ya usalama katika kaunti hiyo inapaswa kuimarishwa vilivyo ili wenyeji waishi bila hofu yoyote.
Vilevile Nassir amesema anapanga kuandaa vikao na wakaazi kila Wadi kaunti ya Mombasa kusikiza maoni kutoka kwao kuhusiana na maduka ya uuzaji vileo yaliyokaribu na makaazi yao ambapo wakaazi wengi wamelalamikia.
Kwa upande wake kamishna wa kaunti ya Mombasa John Otieno amewataka Viongozi wote kushirikana ili kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya na utovu wa usalama.
Wakati huohuo mbunge wa Kisauni kaunti ya Mombasa Rashid Juma Bedzimba ametaja Eneo bunge la Kisauni lenye Wadi 7 kuwa eneo ambalo limekumbwa na matukio mengi ya kihalifu na kutaka Vijana wanaojihusisha na visa vya uhalifu kukabiliwa vilivyo.