Kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyagi amesema idara ya usalama kwenye kaunti hiyo inaendelea kuweka juhudi ili kuwakabili walanguzi wa dawa za kulevya kaunti ya Kwale.
Akizungumza kwenye kaunti hiyo Oyagi amewataka Wazazi kushirikiana na asasi za usalama na taasisi zingine za serikali ili kufanikisha hilo.
Kwa mujibu wa Oyagi iwapo wazazi watajukumika ipasavyo katika kuwalea watoto wao katika maadili visa vya watoto kiunga na magenge ya kihalifu na pia kujihusisha na utumizi wa dawa za kulevya vitakuwa vimedhibitiwa vilivyo.
WIZARA YA USALAMA KAUNTI YA KWALE KUWAKABILI WALANGUZI WA DAWA ZA KULEVYA

