Kamishna wa kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema wamelazimika kuwahamisha wanafunzi 28 wa darasa la 6 kutoka maeneo ya Boni kwa kutumia ndege ya kijeshi hadi kwenye shule ya upili ya Faza ili kufanyia mtihani wao wa KPSEA shuleni humo.
Macharia amesema kwa ushirikiano na wizara ya usalama wameweka mikakati thabiti kuhakikisha wanakabiliana na masuala ya dharura kama vile visa vya wasichana kujifungua wanapoendelea na mitihani yao ya darasa la 8 na ya Gredi ya 6.
Watahiniwa 3,660 wanafanya mtihani wa darasa la 8 na 3,873 wakifanya ule wa Gredi ya 6 kaunti ya Lamu.
KAMWANAFUNZI 28 WA DARASA LA 6 KUTOKA MAENEO YA BONI WAPELEKWA KWENYE SHULE YA UPILI YA FAZA

