Sherehe za kuonyesha utamaduni kisiwani Lamu zinaendelea huku maonyesho mbalimbali yakipangiwa kwenye sherehe hizi za kila mwaka.
Hii ni mara ya kwanza kwa sherehe hizi kufanyika kwa muda wa miaka mitatu baada ya kuathirika kutokana na tandavu ya corona.
zaidi ya wageni elfu 30 tayari wamewasili katika kaunti hiyo ya Lamu huku wakaazi wakisema kuwa tamasha hilo ni afueni kwao kwani litawasaidia pakubwa katika kukua kiuchumi
Ni kauli iliyoungwa mkono na balozi wa Sudani kusini Kamal Gubara sambamba na gavana wa kaunti hiyo Issa Abdallah Timmamy ambaye amesema kuwa sherehe hizo za kitamaduni zitasaidia sana kuimarisha kaunti hiyo kiuchumi.
SHEREHE ZA KUONYESHA UTAMADUNI KISIWANI LAMU ZIMEINGIA SIKU YA PILI LEO

