Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Mung’aro ameseme wamebuni kitengo maalum ambacho kitakuwa kikifuatilia shughuli zote za miradi ya kaunti ya Kilifi ili kuhakisha inatekelezwa kama ilivyokuwa imeratibiwa.
Kulingana na Mung’aro ni kitengo ambacho kitasaidia katika kukabiliana na visa vya ufisadi kwenye miradi ambayo inafanywa na serikali ya kaunti ya Kilifi.
Ametaja visa hivyo kuwa miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikichangia kwa miradi mingi kulemazwa.
Vilevile, amedai baadhi ya watu ambao wamekuwa wakipewa zabuni hizo wamekuwa wakitoa pesa kwa maafisa wa serikali ya kaunti ya Kilifi ili kupata malipo yao baada ya zabuni hizo kukamilika na kuitaja hatua hiyo kuwa kinyume cha sheria.
Akizungumzia utoaji wa Zabuni, Gavana Mung’aro ameahidi zitatolewa kwa wenyeji wote bila kumbagua yeyote.
SERIKALI YA KAUNTI YA KILIFI YABUNI KITENGO MAALUM CHA KUFUATILIA SHUGHULI ZOTE ZA MIRADI YA KAUNTI

