RAILA ODINGA APUZILIA MBALI MGOGORO UNAOKUMA AZIMIO LA UMOJA ONE KENYA

Kinara wa azimio la umoja one kenya Raila Odinga amepuuzilia mbali mgogoro wa kisiasa unaokumba azimio la umoja kwa sasa huku akiwataka viongozi wa vyama tanzu kwenye muungano huo kujadili maswala ibuka wiki hii.
Kwa mujibu wa Raila, cheche za maneno baina ya viongozi katika muungano huo wa azimio la umoja hazisaidii kustawisha upinzani huku akisisitiza kuwa wale wanaotoa cheche hizo wanamlaumu yeye ilhali uchaguzi wa Agosti haukuwa wake binafsi.
Kauli ya Raila inajiri wakati ambapo baadhi ya viongozi wa Jubilee wanaonyesha dalili za kuuhama muungano wa azimio la umoja one Kenya.
Hatahivyo katibu mkuu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni amekubali kuwa upo mtafuruku mkubwa ndani ya azimio la umoja hasa baada ya jubilee kukosa nafasi za uongozi akisema kuwa wenzao katika ODM wamewatenga.
Naye katibu mkuu wa ODM,Edwin Sifuna amesema kuwa jubilee haikutimiza ahadi zake za kuhakikisha kuwa inazoa kura nyingi katika eneo la mlima Kenya.