Mshambuliaji nguli wa timu ya taifa ya ureno mwite Christiano Ronaldo amelalamikia kudharauliwa na klabu yake ya sasa Manchster united. Anasema mkufunzi mpya Erick ten Hag amekuwa akimbagua na kutosikiliza mchango wake kwa timu kama mchezaji mkongwe katika klabu hiyo.
Ronaldo amekuwa na kiwango kibovu msimu huu ikizingatiwa kwamba chini ya mkufunzi mpya ronaldo ameanza mara nne pekee na kuingia mara sita akitokea benchi.
Christiano mwenye umri wa miaka 37 kandarasi yake ya sasa old trafford inatamatika mwezi juni mwaka 2023 na anafuatiliwa na klabu ya Napoli lakini pia Atletico Madrid, hata hivyo katika siku za hivi karibuni mabosi wa chelsea wamekuwa wakinyatia kunasa saini yake.

