HIMIZO LATOLEWA KWA WANANCHI NA ASASI ZA SERIKALI KUENDELEA KUDUMISHA AMANI

Wananchi, asasi mbalimbali za serkali na wadau wamehimizwa kuzingatia amani iliyoshuhudiwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu wa 2022.
Haya ni kwa mujibu wa afisa kutoka kamati ya utekelezaji wa amani kitaifa benard Gitau ambaye amewapongeza wananchi kwa kuzingatia amani na utulivu kwenye uchaguzi uliokamilika mwezi wa nane.
Akizungumza katika kongamano la kutathmini mbinu zilizotumika kudumisha amani, Gitau amesisitiza haja ya idara ya usalama na wananchi kushirikiana katika kuhakikisha imani inadumishwa kwenye maeneo yao
Kwa upande wake afisa mkuu wa utawala eneo la changamwe Nicholus kaito ameihimiza serikali kuiwezesha zaidi kamati ya kutekeleza amani ili iendelee kuhamasisha wananchi kuhusiana na umuhimu wa kuzingatia amani.