MALKIA STRIKERS WAPATA UDHAMINI WA MILIONI 9

Timu ya taifa ya mpira wa wavu Malkia Strikers sasa wanalenga kuanza matayarisho ya michezo ya olimpic itakayo fanyika mjini Paris Ufaransa mwaka 2024 baada ya kuwa na matokeo dunia katika mashindano ya kombe la dunia yalofanyika katika taifa la Poland lakini pia Uholanzi mwaka huu.

Kocha Paul Bitok aliyasema hayo baada ya kupokea udhamini wa milioni 9 kutoka kwa kamati ya Olimpiki Kenya ambazo kulingana na mkufunzi huyo watazitumia vilivyo ili kuwawezesha kuwa na kiwango kizuri wakianza na mashindano yatakayofanyika nchini Ghana mwaka ujao ambayo wanalenga kuyatumia kujipima kabla ya olimpiki za Paris nchini Ufaransa.

Ni kauli iloungwa mkono na Mercy Moim mchezaji wa Malkia strikas ambaye amesema hela za kuwapiga jeki kutoka kwa kamati zitawasaidia sana lakini pia kuwatia motisha kufanya vyema uwanjani.