Mashindano ya kombe la dunia mwaka huu kule QATAR yanatarajiwa kuwa ya mwisho kwa nguli wawili wa soka katika dunia ya sasa ambao ni Messi na Ronaldo ambao kulingana na semi zao za awali huenda wasishiriki mashindano ya kombe la dunia baada ya haya ikizingatiwa kwamba umri utakuwa umekwenda.
Ronaldo atakuwa na umri wa 41 wakati messi akiwa na 39 na Taji hilo la kombe la dunia ndio taji linalowindwa sana baina ya washindani hawa ambao wanasalia kulitamani wakilinganishwa na pele wa brazil aliyelishinda mara tatu pamoja na diego maradona wa Argentina aliyelishinda mara moja mwaka 1986.
Messi na Ronaldo ndio wachezaji wanaokwenda katika mashindano haya ya Qatar wakiwa na wasifu nzuri kama wachezaji binafsi ikizingatiwa kwamba wameshinda Ballon Dor mara 12 baina yao pamoja na makombe manane ya Uefa katika ngazi za klabu.

