Waziri wa uchukuzi wa Kipchumba Murkomen ameweka hadharani nyaraka za mradi mkubwa wa reli ya kisasa SGR uliotiwa saini na China baada shughuli hiyo kuendeshwa kwa usiri kwa miaka kadhaa.
Reli ya thamani ya DOLA bilioni 3 inayofadhiliwa na China ni mradi mkubwa zaidi wa miundombinu humu nchini reli inayopita kati ya mji wa bandari wa Mombasa na mji mkuu, Nairobi, na kuna mipango ya kuupanua hadi mji wa bandari wa Kisumu magharibi mwa Kenya.
Kuweka wazi maelezo ya kandarasi hiyo ya reli ilikuwa mojawapo ya ahadi za Rais William Ruto katika kampeni ili kumaliza uvumi miongoni mwa Wakenya kuhusu kile ambacho serikali ilitia saini kwa niaba yao.
Katika ujumbe wake wa twitter, waziri Kipchumba Murkomen alisema nakala za makubaliano hayo ziwasilishwa kwa viongozi kadhaa katika bunge na pia kusambazwa na vyombo vya habari.
MURKOMEN AWEKA HADHARANI NYARAKA ZA MRADI WA SGR

