Mkufunzi mkuu wa klabu ya Totenhum Hotspurs Antonio Conte amesema anaimani kwamba mchezaji wake Son Hoeng-min atacheza katika mashindano ya kombe la dunia ambako timu yake ya taifa Kosea Kusini inashiriki.
Son ambaye ashafanyiwa upasuaji usoni na anazidi kupata matibabu alipata jeraha hilo alipogongana na Chancel Mbemba, kwenye mechi ambayo Spurs walishinda mabao 2-1 dhidi ya Marceille kunako ligi ya mabingwa ulaya.
Son anasalia kuwa kiungo muhimu katika timu yake ya taifa kutokana na umahiri wake wa kuchana nyavu za mpinzani ikizingatiwa kwamba msimu ulopita alishinda kiatu cha dhahabu sawa na Mohamed Salah wa Liverpool.
Kufikia sasa Son amefungia timu yake ya taifa mabao 34 na ameshiriki mechi 104 akivaa uzi wa Korea Kusini.

