SALIM MVURYA ASEMA SERIKALI KUU IMEWEKA MIKAKATI KUIMARISHA SEKTA YA UVUVI

Waziri wa madini na uchumi wa raslimali za baharini BLUE ECONOMY Salim Mvurya amesema wameweka mikakati thabiti ambayo itasaidia katika kuimarisha sekta ya uvuvi na pia kuboresha kipato cha nchi.
Mvurya ambaye alikuwa akizungumza kwenye kaunti ya Mombasa, amesema serikali kuu inapania kuimarisha shughuli za uvuvi pamoja mazingira ya uvuvi baharini.
Kwa mujibu wa Mvurya Mikakati zaidi ya kuimarisha sekta ya uvuvi inaendelezwa ili kuhakikisha wavuvi nchini Kenya wanakuwa na nafasi zaidi ya kuvua samaki katika maeneo ya katikati mwa bahari hindi ya Kenya.
Vilevile, amesema tayari serikali kuu imetenga maeneo ambayo yatawekezwa bandari ndogo ndogo za kuhifadhia vifaa vya uvuvi pamoja na maeneo ya kuhifadhia samaki pembezoni mwa bahari.