TAKRIBANI SHULE 180 KAUNTI YA TANA RIVER KUNUFAIKA NA CHAKULA CHA MSAADA

Mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Tana River Khalif Hassan amesema takribani shule 180 za msingi kwenye kaunti hizo zinatarajiwa kunufaika na chakula cha msaada kutoka kwa serikali ya kitaifa.
Katika taarifa yake kwa waandishi wa habari amesema chakula hicho kimeanza kuwasili kwenye kaunti ya Tana River.
Amesema chakula zaidi cha msaada kikitarajiwa kuwasili na kuwafaidi wanafunzi hasa walioko kwenye maeneo kame .
Aidha, amesema kupitia mpango huo wa chakula cha msaada kwa shule mbalimbali katika kaunti ya Tana River utachangia kuwawezesha wanafunzi kuhudhuria masomo yao bila changamoto zozote.