HIMIZO LATOLEWA KWA WENYEJI WA TANA RIVER KUPANDA MITI NA NYASI

Wakaazi wa Tana Delta kaunti ya Tana River wameshauriwa kupanda miti na nyasi kwa wingi wakati huu ambapo kumeanza kushuhudiwa mvua baada ya kipindi kirefu cha kiangazi.
Mshirikishi wa shirika la NATURE KENYA George Odera amesema wakaazi wa Tana River walikua na wasiwasi wa kupoteza mifugo wao kutokana na ukosefu wa malisho na maji hali iliyosababisha kukata miti kwa ajili ya kupatia mifugo wao lishe.
Odera amewashinikiza wakaazi kupanda miti na nyasi kwa minajili ya kudumisha mazingira bora sawia na kupata chakula cha mifugo wao siku za usoni lakini pia amewataka wakulima kutayarisha mashamba yao kabla ya upanzi wa mimea inayokua kwa haraka.