WANAOJIHUSISHA NA UWINDAJI HARAMU ENEO LA MPEKETONI WAONYWA

Msimamizi wa masuala ya wanyamapori kaunti ya Lamu Mathius Mwavita amewaonya vijana kwenye kaunti hiyo ambao wanajihusisha na uwindaji haramu wa wanyamapori.
Mwavita amesema baadhi ya vijana eneo la Mpeketoni wamekuwa wakiwawinda wanyamapori na nyama kuuzwa katika masoko yaliyoko eneo hilo.
Amewaonya wale ambao wananunua nyama ya wanyamapori akisema haijakaguliwa na idara husika kubaini iwapo ni salama au la kwani huenda wakaugua magonjwa mbalimbali.
Kwa mujibuwa Mwavita wenyeji ambao watapatikana wakiwinda wanyamapori kama Nyati na viboko watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.