Seneta mteule katika kaunti ya Lamu Shakilla Abdalla amesema kuna haja ya rais William Samoei Ruto kuwapa nafasi za uongozi wenyeji wa kaunti hiyo kwenye ngazi za kitaifa ili kaunti hiyo iweze kuwakilishwa kiukamilifu.
Amesema katika serikali kuu bado kuna nafasi za makatibu wakuu na mabalozi ambazo zimesalia hivyo basi wenyeji wa kaunti hiyo wanapaswa kukumbukwa.
Kulingana na Shakilla aliyekuwa mbunge wa Lamu Mashariki Shariff Athman Ali ambaye alishindwa kwenye kipute hicho katika uchaguzi uliondaliwa Agosti 9 mwaka huu wa 2022 kupewa nafasi ya uongozi akisema amekuwa mstari wa mbele kumfanyia kampeni Rais Ruto.
SHAKILLA ABDALLA AMTAKA RAIS RUTO KUWAPA WATU WA LAMU NAFASI ZA UONGOZI

