MISHI MBOKO AIKOSOA SERIKALI KUU

Mbunge wa Likoni kaunti ya Mombasa Mishi Mboko ameikosoa serikali kuu kutokana na kile ambacho anadai imekosa kuwateua watu wenye uatilifu katika baraza la mawaziri nchini.
Kulingana na Mboko idadi ya watu wenye uwezo maalumu nchini ni kubwa katika taifa hili na ingekuwa vyema iwapo kungeteuliwa mmoja wao ambaye atawawakilisha ipasavyo.
Mishio Mboko ambaye alikuwa akizungumza kwenye eneo bunge lake katika halfa iliyowaleta pamoja watu wenye uatilifu amesema walipaswa kuwa na mtu mmoja atakayewasilisha matakwa yao ili yatekelezwe kiukamilifu.
Akizungumzia hazina ya HUSTLER FUND ameitaka serikali kuu kuwatengea mgao ambao utawawezesha watu wenye uatilifu kujikimu kimaisha…
Kauli yake imeungwa mkono na mwakilishi wa kike katika kaunti ya Mombasa Zamzam Mohamed ambaye amewahimiza viongozi nchini kuhakikisha wanawapa ajira watu wenye uwezo maalum ili waendelee kujiendeleza maishani.