Naibu gavana wa kaunti ya Kilifi Margaret Chibule amesema kaunti ya Kilifi sasa imeanza kushuhudia ongezeko la idadi ya watoto, wanaopachikwa ujauzito wakiwa chini ya umri wa miaka 13.
Naibu gavana huyo amethibitisha kupokea taarifa za watoto watano waliochini ya umri huo, ambao wamepata ujauzito katika sehemu mbalimbli za kaunti ya Kilifi.
Akizungumza katika eneo bunge la Ganze, amewaonya wale wanaowapachika mimba watoto hao na kusema watakaopatikana watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.
Wakati huohuo amesema serikali ya kaunti ya Kilifi inaendeleza mikakati ya kutekeleza ujenzi wa kituo cha kukuza vipaji na talanta za vijana kaunti ya Kilifi na kusema ni njia mojawapo ya kukabiliana na visa vya vijana kujiunga na magenge ya kihalifu na utumizi wa dawa za kulevya kutokana na kutokuwa na kitu cha kufanya mitaani.
KAUNTI YA KILIFI YAANZA KUSHUHUDIA ONGEZEKO LA MIMBA ZA UTOTONI

