WENYEJI WA TANA RIVER WANATARAJIA KUSHUHUDIA MIRADI YA MAENDELEO

Waziri wa fedha kaunti ya Tana River Mathew Baboya emesema serikali ya kaunti hiyo kwa sasa iko katika nafasi nzuri ya kutekeleza miradi ambayo itawafaidi wenyeji kwa kiwango kikubwa.
Kwa mujibu wa Waziri huyo anadai katika awamu ya kwanza ya uongozi wa gavana wa kaunti hiyo Dhadho Godhana, serikali hiyo ilikabiliwa na changamoto kutokana na kile ambacho anadai kutokana na malimbikizi ya madeni ambayo yaliachwa na mtangulizi wake.
Aidha, amesema kufikia sasa madeni mengi ya kaunti ya Tana River yamelipwa na wanatarajia kutekeleza miradi mbalimbali kwa wenyeji.