MCHEZAJI WA ARSENAL AVAMIWA ITALIA

Difenda wa klabu ya Arsenal Pablo Mari anapokea matibabu katika hospitali moja mjini Milan Italia baada ya kuvamiwa na kudungwa kisu hapo jana.

Mari pamoja na watu wengine watano walipatikana kwenye uvamini huo walipokuwa kwenye duka la jumla wakinunua bidhaa kabla ya jambazi aliyekuwa amejihami na kisu kufamia duka hilo na kujeruhi wanunuzi.

Kutokana na kisa hicho mtu mmoja mwenye umri wa miaka 30 anaripotiwa kufariki dunia kufuatia majeraha makali aloyapata huku wengine watano wakilazwa hospitali kupokea matibabu mmoja wao akiwemo Pablo Mari ambaye anatarajiwa kufanyiwa upasuaji hii leo.

Kufikia sasa mtu mmoja ameripotiwa kukamatwa kutokana na kisa hicho na anatarajiwa kushtakiwa huku maafisa wa jeshi la polisi wakizidisha uchunguzi zaidi.

Pablo Mari kwa sasa anachezea klabu ya Monza kule italia kwa mkopo akitokea arsenali baada ya kusajiliwa kutoka Flemingo ya Brazil mwaka 2020