MASHINDANO YA SOKA MAGHARINI YAPIGWA KALENDA

Mashindano ya soka ya FKF tawi la eneo bunge la Magharini kaunti ya Kilifi sasa yamepigwa kalenda kwa muda usiojulikanana.

Taarifa kwa vyombo vya habari lakini vilabu imetolewa rasmi na shirikisho hilo kupitia Emmanuel Kazungu amabaye ni katibu wa soka katika eneo hilo huku vilabu 24 kutoka eneo la gongoni vikiachwa mataani kwa sasa wakiwa wengi wa maswali kwa shirikisho hilo kuhusu tukio hilo la ghafla.

Ila taarifa zilizofikia Tama la Spoti kwa sasa ni kwamba wakuu wa FKF eneo bunge hilo wanalenga kuandaa mkutano baina yao wiki ijayo kutafuta mwafaka wa mashindano hayo.

Hadi kusitishwa kwake mashindano hayo bado yalikuwa hayajapata mdhamini wa kuyasimamia huku vilabu awali vikilalamika huenda vingelemewa kusimamia mechi hizo kutokana na ukata wa kifedha uliopo miongoni mwa mashinani.