Muungano wa mabaharia wakongwe kaunti ya Mombasa unapendekeza kuwe na mabadailiko ili kuboresha sekta hiyo.
Kulingana na Mabaharia hao kipengee cha ubaharia kinapaswa kufanyiwa mabadiliko wakidai licha ya kuwa na tajriba ya zaidi ya miaka 15 wengi wao wamesalia bila ajira.
Wanasema iwapo mageuzi hayo yatafanywa itakuwa afueni kwao kwani baadhi yao wanaendelea kuhangaika kutokana na ukosefu wa kazi hali ambayo inaendelea kuwaathiri.
Kulingana nao wamekuwa wakibaguliwa katika masuala ya ubaharia na nafasi za kazi kukabidhiwa vijana.
Wanadai vijana ndio ambao wanachukuliwa na baadhi ya kampuni za meli ili kuweza kuhudumu kama mabaharia kwenye mataifa mbalimbali wakisema vyeti walivyo navyo vimekaa kwa muda mrefu bila ya wao kufanya kazi.
Aidha, wametoa wito kwa rais William Samoei Ruto kufanya baadhi ya mageuzi ambayo yatawawezesha mabaharia wote wanaoelekea ughaibuni kuweza kupokea mafunzo ya kisasa.
MUUNGANO WA MABAHARIA WAKONGWE KAUNTI YA MOMBASA WALALAMIKA

