DAN MWASHAKO ASEMA BAADHI YA MAWAZIRI WATEULE HAWANA TAJRIBA YA KUTOSHA

Mbunge wa Wundanyi kaunti ya Taita Taveta Dan Mwashako amesema baadhi ya mawaziri wateule waliohojiwa na kamati ya uteuzi katika bunge la kitaifa baada ya kupendekezwa na rais William Samoei Ruto hawakuwa na tajriba ya kutosha kama inavyopaswa kulingana nafasi hizo za uwaziri.
Mwashako amesema ni lazima anayeteuliwa kuwa waziri awe na ufahamu wa kina kuhususia na wizara husika.
Akizungumza katika kaunti ya Taita Taveta Mwashako amesema wizara nyingi nchini zimedorora kutokana na kile ambacho anadai kuchangiwa na mawaziri wasiokuwa na tajriba ya kutosha kukabidhiwa nyadhifa za uongozi kwenye wizara mbalimbali.