Naibu kamishna eneo la Wundanyi kaunti ya Taita Taveta Maina Ngunyi amesema serikali kuu inashirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha inakabiliana na janga la Ukame.
Kulingana na Ngunyi vyanzo vingi vya maji vimekauka hali ambayo imekuwa ikisababisha wenyeji kutembea mwendo mrefu kusaka maji safi ya matumizi.
Amesema hali hiyo ya kukauka kwa vyanzo vya maji kunawapa wasiwasi kwani eneo hilo limekuwa na maji ya kutosha tangu zamani.
Vilevile, amesema wameweka mikakati thabiti ili kusambaza maji kwenye maeneo ambayo yana uhaba wa maji.
MAINA NGUNYI ASEMA SERIKALI KUU INASHIRIKIANA NA YA TAITA TAVETA

