WANAFUNZI WANAOLIPIWA KARO NA SERIKALI YA LAMU WAHIMIZWA KUTIA BIDII MASOMONI

Gavana wa kaunti ya Lamu Issa Abdalla Timamy amewataka wanafunzi ambao wako kwenye shule za upili na wanalipiwa karo na serikali ya kaunti hiyo kutia bidii masomoni ili kuendelea kulipiwa karo ya shule.
Amesema ni lazima wanafunzi wajitahidi katika masomo yao iwapo wanataka kuendelea kupata ufadhili huo ili wanufaike na fedha hizo kutoka kwa serikali ya kaunti ya Lamu.
Serikali ya kaunti ya Lamu imewapa ufadhili wa masomo wanafunzi wote wanaopata alama zaidi ya 300 kwenye mtihani wao wa darasa la 8 ambapo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne wanalipiwa karo na serikali ya kaunti hiyo.
Amewataka wazazi kupeleka matokeo ya mitihani ya watoto wao walioko kwenye shule za upili wanaosimamiwa na serikali ya kaunti ya Lamu kila wanapofanya mtihani.