LYDIAH HAIKA AWATAKA WALIMU WAKUU TAITA TAVETA KUTOWAFUKUZA WANAFUNZI

Mwakilishi wa kike kaunti ya Tata Taveta Lydiah Haika amewataka walimu wakuu kuwaruhusu wanafunzi kuendelea na masomo yao licha ya kuwa wanadaiwa karo.
Haika ambaye alikuwa akizungumza kwenye kaunti hiyo, amesema kutokana na hali ngumu ya maisha ambayo inaendelea kuwakabili wananchi wazazi wanapitia wakati mgumu kulipa karo ya watoto wao.
Vilevile, amewataka walimu kuhakikisha masomo yanaendelea kama kawaida na kutaka mzozo kuhusu usimamizi fedha za ustawishaji wa maeneo bunge NG – CDF kuangaziwa akisema wanafunzi wengi ambao wanatoka familia zisizojiweza wamekuwa wakitegemea fedha hizo.