WATU WENYE UWEZO MAALUM KAUNTI YA KILIFI WATAKIWA KUJISAJILI

Watu wanye uatilifu kaunti ya Kilifi wametakiwa kujisajili katika bodi inayosimamia watu wenye uwezo maalum na kupewa vitambulisho maalum ili kunufaika na misaada mbalimbali ya serikali kuu inayowalenga.
Haya ni kwa mujibu wa mwenyekiti wa watu wenye uatilifu kaunti ya Kilifi Jacob Sirya, ambaye amesema iwapo watasajiliwa watanufaika zaidi kwani itakuwa rahisi kwao kupata ufadhili wa masomo na kupewa vitambulisho rasmi vya watu wenye uatilifu.
Sirya ambae pia ni msimamizi wa shughuli za kaunti katika eneo bunge la Kilifi Kaskazini, amesema serikali ya kaunti ya Kilifi inapaswa kubuni mikakati thabiti ya kutekeleza zoezi la usajili wa watu wenye uwezo maalum ili kuhakikisha wanapata data kamili kuhusiana na idadi ya watu uwezo maalum walioko katika kaunti ya Kilifi.
Wakati huohuo amesema kwa sasa hawawezi kutatua matatizo yanayowakumba watu hao kama baa la njaa katika maeneo kame kaunti ya Kilifi kwani hawana takwimu kamili za watu wenye uatilifu wanaokumbwa na baa hilo.
Haya yanajiri huku zoezi hilo likiendeleza katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi.