Gavana wa kaunti ya Kwale Fatuma Achani ametoa wito kwa Jamii kutumia vyema mitandao ya kijamii kwenye masuala ambayo yatawafaidi na sio kuitumia kuwadunisha wanawake ambao wanapania kujiunga na siasa.
Katika taarifa yake kwa wenyeji wa kaunti hiyo, Achani ametolea mfano wa wakati alipokuwa akiendeleza kampeni zake za kuwania wadhifa wa ugavana ambapo baadhi ya wapinzani wake waliwatumia vijana kumkejeli na kumtusi kupitia mitando ya Kijamii.
Aidha, amesema licha ya hayo yote hakusitisha juhudi zake za kuwania wadhifa huo na kushinda kwenye kipute hicho cha ugavana hata baada ya kupitia matusi na kejeli.
Amewataka wanawake kutokatizwa tamaa na baadhi ya watu katika jamii ambao lengo lao ni kuwadunisha na kuwahimiza kujiunga na siasa ili kutimiza ndoto zao za uongozi.
GAVANA ACHANI AWATAKA WANAWAKE KUWEKA JUHUDU ZAIDI KATIKA UONGOZI

