Rais William Ruto amesema kuwa yuko tayari kufanya kazi na kinara wa wiper Kalonzo Musyoka kwa manufaa ya wenyeji wa ukambani ila Kalonzo mwenyewe hajaonyesha nia ya kukubaliana na hatua ya kushirikiana na serikali.
Akizungumza hapo jana katika ibada ya shukrani kwenye kanisa la AIC kaunti ya Kitui, rais Ruto amesema kuwa alichukua hatua ya kufanya mazungumzo na Kalonzo ila kwa mujibu wa rais Kalonzo bado ameshikilia kuwa kiongozi wa upinzani.
Hatua ya rais Ruto imechochewa na shinikizo na viongozi kutoka kwa mrengo wa Kalonzo wakimtaka rais ashirikiane na Kalonzo ili kuiweka jamii ya ukambani kwenye nafasi nzuri serikalini.
Naibu wa rais Rigathi Gachagua pia amekiri kuwa Kalonzo ameonyesha kutokubaliana na shinikizo hizo na badala yake atashikilia kufanya kazi kwenye upande wa upinzani.
RAIS RUTO ASEMA YUKO TAYARI KUFANYA KAZI NA KALONZO MUSYOKO

