IRUNGU MACHARIA AWAONYA WENYEJI DHIDI YA KUSHIRIKIANA NA MAGAIDI

Kamishna wa kaunti ya Lamu Irungu Macharia amesema mikakati thabiti imewekwa na asasi za usalama katika kaunti hiyo ili kudhibiti visa vyovyote vya utovu wa usalama.
Katika hotuba yake kwa wenyeji wa kaunti hiyo, Macharia amewaonya magaidi wa Al – Shabaab ambao wanapania kutekeleza mashambulizi kwenye kaunti hiyo na kusema idara ya usalama imejiandaa katika kuwakabili.
Macharia amewaonya wenyeji dhidi ya kushirikiana na Magaidi wa Al – Shabaab kutekeleza mashambulizi kaunti ya Lamu.
Kwa upande wake gavana wa kaunti hiyo Issa Abdalla Timamy amewataka maafisa wa usalama kutowahangaisha wageni ambao wanazuru kaunti hiyo.