Viongozi wa soka la mashinani wanasema kwamba vijana wengi kwa sasa wanazidi kusajili timu zao kucheza ligi za mashinani jambo linalotajwa kuwa michezo hasa wa soka unazidi kupendwa na mashabiki lakini pia vijana.
Akizungumza na tama la spoti katribu wa soka la eneo bunge la maghatrini mwote Emmanuel kazungu amesema kuwa kwa sasa kunako ligi la eneo lake, vilabu vingi vimeshajisajili wanaposubiri msimu mpya wa mwaka 2022/2023.
Kazungu anasema kuwa licha ya ongezeko ya vilabu hivyo ameshauri wakuu wa timu zote kujitayarisha kifedha wanaposubiri tarehe rasmi ya kuanza kwa msimu mpya ambao taarifa inayosubiriwa ni kutoka kwa FKF ya Nick Mwendwa.

