BALOZI WA UJERUMANI AMEAHIDI USALAMA UTAIMARISHA KWENYE FUO ZA BAHARI PWANI

Balozi wa Ujerumani nchini Kenya Sebatian Groth amesema mikakati imewekwa ya kuimarisha usalama katika fuo za bahari na maeneo ya kitalii kanda ya pwani.
Akizungumza na wanahabari katika makao makuu ya polisi kaunti ya Mombasa amesema hawana hofu kuhusu usalama wa taifa hili na kuahidi kutakuwa na wageni kutoka Ujerumani ambao watazuru nchini Kenya.
Kulingana na Sabastian wanatarajia idadi ya wageni kutoka taifa la Ujerumani kuongezeka hasa wakati huu tunakaribia msimu wa Krismasi na mwaka mpya.
Wakati huohuo Balozi Groth amesema pikipiki 10 ambazo wamezitoa kwa kitengo cha polisi kuhusu utalii zitasaidia pakubwa kuimarisha usalama kwa watalii wanaofika katika fuo mbalimbali za bahari kanda ya Pwani.
Kwa upande wake kamanda wa polisi katika kitengo cha utalii nchini Paul Soi amesema wameweka mikakati thabiti kuhakikisha hakuna utovu wowote wa usalama unashuhudiwa.