Waziri wa kilimo katika serikali ya kaunti ya Tana River Pharis Buya amewataka wenyeji kuanza kutumia kilimo cha Kunyunyiza maji kwa kutumia kawi ya jua akisema mabadiliko ya hali ya anga yameathiri misimu wa kushuhudiwa mvua.
Buya amesema imekuwa vigumu kutabiri mvua kwani kuna wakati zinachelewa au hata kukosa kushuhudiwa hali ambayo imekuwa ikichangia kushuhudiwa kwa kiangazi.
Akizungumza kwenye kaunti hiyo amesema iwapo wenyeji watazingatia mfumo huo huenda suala la baa la njaa likadhibitiwa kwa kiwango Fulani.
Naye Abdi Musa ambaye ni mshirikishi wa mamlaka ya kukabiliana na ukame katika kaunti hiyo amesema kuna haja ya mipango thabiti kuwekwa ili kuwe na mavuno ya kutosha katika kaunti ya Tana River.
WENYEJI WA TANA RIVER WATAKIWA KUTUMIA KILIMO KUNYUNYIZA MAJI KWA KUTUMIA KAWI YA JUA

