Klabu ya Real Madrid kule Uhispania iliitandika klabu ya Barcelona katika mtanange maarufu wa El clasico uliofanyika dimbani Santiago Barnebou uliotamatika kwa vijana na Carlo Ancelloti kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Bao la mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa Karim Benzema, goli la Fede Valverde na lile la kinda wa Brazil Rodrigo katika dakika za lala salama kupitia mkwaju wa penanti ndio yalotosha kuwapa ushindi Real Madrid.
Kwa upande wao Barcelona nguvu mpya Ferran Torres ndiye aliyeipa Barca bao la kufutia machozi.
Kwa matokeo hayo hapo jana sasa Real Madrid imekwea kileleni mwa Laliga na alama 25 wakati Barcelona ikisimama katika nafasi ya pili na alama 22.

