KOCHA WA MALKIA STRIKERS AMPENDEKEZEA NAIBU SPIKA MSWADA WA KULINDA WACHEZAJI

Kocha mkuu wa kikosi cha kinadada Malkia Strikers mwite Paul Bitok hapo jana alifanya mazungumzo na naibu spika wa bunge la kitaifa Gladys Sholei, mazungumzo yaliyolenga kupeleka misuada bungeni ya kulinda wachezaji wanaotumikia taifa hili na kuletea mafainikio mengi kuanza kulipwa malipo ya uzeeni wachezaji hao wanapo staafu.

Mkutano huo unafanyika baada ya Paul Bitok kurejea nchini kutoka kwenye mashindano ya dunia ya mpira wa wavu na kinadada malkia strikers mashindano yalofanyika nchini Poland lakini pia uholanzi.

Malkia strikers walitolewa katika hatua ya makundi baada ya kusajili ushindi mmoja pekee na ilikuwa dhidi ya Camerroon.

Paul Bitok ameiomba serikali kuenzi wachezaji wakongwe walioletea taifa hili jina na kuiweka Kenya kwenye ramani ya dunia.