MRADI WA UTOAJI CHAKULA KWA SHULE ZA CHEKECHEA KUANZISHWA TANA RIVER

Afisa mkuu wa idara ya elimu katika serikali ya kaunti ya Tana River Fatuma Bona Gafo wataendeleza mradi wa utoaji chakula kwa shule za chekechea baada ya kukwama kwa muda tangu ujio wa janga la virusi vya Corona nchini.
Bona amesema tayari sera zimebuniwa kwa elimu ya chekechea ambazo zitatoa muongozo bora katika shule hizo ili wanafunzi waweze kusoma bila kutatizika.
Amesema mwaka huu wa 2022 ndio ambao serikali imeweza kufanikiwa kutekeleza mpango huo ambao ameutaja kuwa wenye manufaa kwa wanafunzi wa chekechea.