Mwenyekiti wa maonyesho ya Kilimo kanda ya pwani Anisa Abdalla amesema mbinu ya ukuzaji vyakula kupititia kisayansi GMO itaangaziwa wakati wa maonyesho ya kilimo ya mwaka huu katika kaunti ya Mombasa.
Kauli yake inajiri kufuatia madai kuwa mbinu hiyo itachangia kwa wananchi kukumbwa na madhara mbalimbali kama kuugua ugonjwa wa saratani hali ambayo inaendelea kuibua hisia mseto miongoni mwa wakenya na viongozi.
Maseneta wanaogemea muungano wa Azimio la Umoja One Kenya wanaendelea kukosoa hatua ya Rais William Samoei Ruto ya kuruhusu nchini vyakula vinavyokuzwa kisayansi (GMO) baada ya kuondoa marufuku iliyotangazwa 2012 dhidi ya ukuzaji na uagiziaji wa vyakula vya GMO nchini.
Hatua hiyo illifanya Kenya kuwa taifa la pili baada ya Afrika Kusini kuidhinisha vyakula vilivyokuzwa kisayansi Barani Afrika.
ANISA ABDALLA ASEMA MBINU YA UKUZAJI VYAKULA KUPITIA MBINU YA GMO ITAANGAZIWA

