wenyekiti wa vuguvu la AMKENI COAST MOVEMENT Farida Rashid pamoja na wanaharakati wenza wamewakosoa wanaopinga kuondolewa mashtaka kwa aliyekuwa mbunge wa Malindi kaunti ya Kilifi Aisha Jumwa.
Farida ametoa wito kwa wanaopinga hatua hiyo kuwasilisha lalama zao kwa mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Noordin Hajji na sio kuibua kashfa ambazo hazina misingi yoyote.
Katika taarifa yake akiwa kaunti ya Mombasa amesema kupendekezwa kwa Aisha Jumwa kwa waziri wa utumishi wa umma sio kinyume cha sheria.
Aidha, amesema anaamini iwapo Aisha Jumwa ataidhinishwa kuwa waziri atatekeleza majukumu yake ipasavyo na kuwaonya wanaomkejeli na kumshutumu kwa madai mbalimbali.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na mwanaharakati wa vuguvugu hilo Margret Kisiengo almaarufu kama Ambassa na kuwataka wakenya kushirikiana na viongozi ili kufanikisha miradi ya maendeleo nchini.
Haya yanajiri baada ya mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma nchini Noordin Hajji alieleza mahakama ya Mombasa kuwa alikuwa na nia ya kuondoa mashtaka ya ufisadi dhidi ya Aisha Jumwa.
VUGUVUGU LA AMKENI COAST MOVEMENT YAMTETEA AISHA JUMWA

