KECOSCE YAWATAKA VIONGOZI WA DINI TANA RIVER KUENDELEA KUHAMASISHA WENYEJI UMUHIMU WA KUDUMISHA JAMII

Afisa katika shirika la kushughilikia amani na usalama katika jamii KECOSCE Maxwell Lumbasi, amewahimiza viongozi wa dini kuwa mstari wa mbele kuwahimiza wenyeji wa Tana River kudumisha amani.
Akizungumza katika mkutano uliowaleta pamoja washikadau mbalimbali wa masuala ya Amani kutoka mashinani, Lumbasi amesema dini inaweza kutumika kuwahamasisha wananchi umuhimu wa kudumisha kwa jamii.
Aidha, amewapongeza viongozi wa dini kwa kujishughulisha katika masuala mbalimbali, kama kuunda sera na pia utekelezaji wa miradi katika jamii, ambayo imekuwa yenye manufaa kwa wenyeji.