Gavana wa kaunti ya Kilifi Gideon Maitha Mung’aro amesema kuna madaktari zaidi ya 15, ambao wameendelea kupokea mshahara licha ya wao kutokuwa kazini.
Kwa mujubu wa gavana huyo madakatari hao wanadaiwa kuchukua likizo ya kuendeleza masomo yao kwa miaka mitatu, jambo ambalo anadai kutokuwa la kweli.
Mung’aro amesema tayari madaktari hao wamepokea ilani ya kurudi kazini baada ya wiki mbili na kusema kuwa iwapo hawatarudi serikali ya kaunti italazimika kuwafuta kazi.
Wakati uohuo amesema wale waliolipiwa karo na serikali ya kaunti ya Kilifi watalazimika kurudisha fedha zilizotumika ama kulazimika kufanya kazi kwa miaka mitatu kabla ya kupewa barua ya uhamisho.
GEDION MUNG’ARO ATOA ILANI KWA MADAKTARI 15 KAUNTI YA KILIFI

