Mbunge wa Changamwe kaunti ya Mombasa Omar Mwinyi ametoa wito kwa serikali kutoingiza siasa katika utendakazi wa bandari ya Mombasa.
Amewataka viongozi katika bandari hiyo kuachwa watekeleze majukumu yao kikamilifu, kwa ajili ya kupanua utendakazi wa bandari hiyo.
Akizungumza na vijana katika eneo la Changamwe kuhususiana uchumi wa raslimali za baharini BLUE ECONOMY, Mwinyi amesema iwapo bandari ya Mombasa itaendeleza shughuli zake bila kuingiliwa na serikali, uchumi wa kaunti ya Mombasa na taifa la Kenya kwa jumla utaimarika zaidi na hata nafasi za ajira kubuniwa.
Hata hivyo ametoa wito wa kukamilishwa chuo cha utalii cha Ronald ngala katika kaunti ya kilifi, ili kuwapa fursa vijana wa pwani kupata ajira.
OMAR MWINYI ATAKA SIASA KUTOINGIZWA KATIKA UTENDAKAZI WA BANDARI YA MOMBASA

