CHRISTIANO RONALDO SASA AMEINGIA KAMBANI MARA 700

Nguli wa soka Cristiano Ronaldo sasa amefikisha magoli 700 tangia kuanza rasmi kusakata soka la ushindani na kulipwa katika klabu yake ya ujanani Sporting Lisbon kabla ya kwenda klabu nyingine. Ametimiza idadi hiyo baada ya kufunga bao moja kwenye mechi ya ushindi wa bao 2-1 dhidi ya Everton usiku wa kuamkia leo.

Christiano Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 amekuwa akikosolewa katika siku za hivi karibuni kufuatia kiwango hafifu cha mchezo wake pale Manchester United na alifunga bao hilo akitumia pasi safi ya Casemiro dakika 15 baada ya kuingia uwanjani akitokea benchi na kuchukua nafasi ya Anthony Martial.

Ronaldo bao lake la kwanza alifunga mwaka 2005 kabla ya kwenda Manchester United kisha Real Madrid, Juventus na kurejea tena Manchester United.