KINA MAMA KAUNTI YA TANA RIVER WATAKIWA KUWATOA NJE WATOTO WAO WACHANGA

Afisa anayesimamia kitengo cha wauguzi kwenye hospitali ya Garsen kaunti ya Tana River Hassan Roba ametoa wito kwa kina mama kuwatoa nje watoto wao wachanga baada ya kuzaliwa.
Amesema hatua ya baadhi ya kina mama kukosa kuwatoa nje watoto wachanga baada ya kuzaliwa inahatarisha afya ya mtoto wao.
Kwa mujibu wa Roba desturi ya watoto wachanga kukosa kutolewa nje kwa siku 40 baada ya kuzaliwa kunamchelewesha mtoto wengi kupata chanjo mapema, hali ambayo inawaweka kwenye hatari ya kuugua magonjwa mbalimbali.
Amewahimiza kina mama kuhakikisha watoto wao wanachanjwa kulingana na ilivyoratibiwa na madaktari ili kuwaepusha dhidi ya kuugua magonjwa.
Akigusia suala la upangaji uzazi, Roba amewataka kina mama kuzingatia mbinu za upangaji uzazi akisema hatua hiyo itasaidia kuwaepusha wototo wao dhidi ya kuugua ugonjwa wa utapyamlo.