WANAHARAKATI TAITA TAVETA WASEMA WENYEJI HAWAFAHAMU MIPAKA YA MASHAMBA YAO

Wanaharakati wa masuala ya ardhi kaunti ya Taita Taveta wanasema kuna haja ya kutumia ardhi nchini ili kutoa ramani mbalimbali za ardhi kwenye kaunti hiyo ili wenyeji waweze kufahamu mipaka yao halisi.
Wakiongozwa na Chris Mwambingu wanasema licha kuwa wenyeji wamekuwa wakikabidhiwa hati miliki zao, wengi wao hawajui mahali kwenye ardhi hizo ziko kwa madai mara nyingi zinakosekana.
Amesema ili kudhibiti migogoro ya ardhi ni sharti serikali ya kaunti hiyo iendeleze zoezi la kupima ardhi hasa katika eneo bunge la Mwatate.